Vera Sidika na Otile Brown Wathibitisha Kurudiana

Socialite maarufu kutoka Kenya Vera Sidika ‘Queen Vee’ na mpenzi wake Msanii wa muziki Otile Brown wamethibitisha kkurudiana baada ya kuachana mapema mwezi jana.

Vera na Otile walikuwa Kwenye Mahusiano kwa Miezi michache lakini walianika Penzi lao Kwenye mitandao ya kijamii kwa sana na hata Vera kuwa video queen Kwenye moja ya video za nyimbo ya Otile.

Wawili hao walitangaza kumwagana mwezi iliopita huku kila mmoja akimnyooshea kidole mwenzake kama kuwa chanzo cha Penzi lao kuvunjika.

Tetesi za wawili hawa kurudiana zilianza kutawala siciao Media wiki hiii baada ya Vera na Otile kukutana Dubai, Lakini sasa kila mmoja amethibitisha Kurudiana baada ya kuposti Kwenye mitandao ya kijamii:

Lakini pia wawili hao wameweka video mbali mbali Kwenye mitandao ya kijamii zinazowaonyesha wakiwa wanakula bata Dubai na kuzima taarifa zote za kuachana.